Oscar Sudi, Kositany na Kiplangat washtumiwa kuharibu Ndege ya Raila

Kindly read and share to support us reach our target audiences.
Embakasi East MP Babu Owino shares vandalised Azimio-OKA presidential flagbearer Raila Odinga’s chopper which was stoned on Friday 01/04/2022 at Mzee Kibor’s burial. Photo:Source/Twitter-Facebook

Mbunge wa Kapsaret Oscar Sudi na mwenzake wa Soy Mbunge wa Soy Caleb Kositany na spika wa Uasin Gishu David kiplangat wanashukiwa kupanga njama ya kuharibu ndege ya kibara wa ODM Raila Odinga

Watatu hao wametakiwa kujisalimisha katika kituo cha polisi jumatatu ijayo kujibu tuhuma za uchochezi na kufadhili vijana kupiga mawe ndeye ya kinara wa Azimio

Tayari watu 17 walitiwa mbaroni baada ya kisa hicho kichotendeka Ijumaa katika mazishi ya mfanyibiashara na mwanasiasa mashuhuri Jackson Kibor na wanaendelea kuhojiwa

Wakati uo huo Waziri wa usalama Fred Matiang’i alitaka uchunguzi wa haraka kufanyika

Wanawe marehemu Jackson kibor waliomba msamaha kwa kile kilotendekea kiongozi huyo wa chungwa

Watakaopatikana na makosa watafunguliwa mashtaka ya uchochezi na uharibifu wa mali ya umma na ya kibinafsi

Hata hivyo mbunge huyo wa Kapsaret alikanusha kupanga njama hiyo na kuwataka vijana waliotenda kitendo hicho kuchukuliwa hatua

Oscar Sudi’s take on social media. Photo: Twitter source:Facebook

Aliyasema hayo katika mitandao ya kijamii