Wabunge Wafurusha Wanahabari Bungeni

Kindly read and share to support us reach our target audiences.
Mbunge wa Kitui Kusini Daktari Racheal Nyamai. Picha|Screengrab|

Mbunge wa Kitui Kusini Rachael Nyamai amewakashifu wanahabari wanaoripoti masuala ya bunge kwa kile amekitaja kama “mwenendo wao kuvalia mavazi ya aibu wakiwa katika majengo ya bunge”.

Akizungumza huko Mombasa katika mkutano wa wabunge hiyo jana, Bi Nyamai, alidai watazungumza na wahusika ili kurekebisha tabia hiyo

“Inaonekana kuna hitilafu kuhusu namna bunge huendesha shughuli zake haswa kuhusiana na mavazi ya watu na kundi kubwa ya wanahabari tulio nao bungeni. 

Tungependa kufanya mazungumzo na uongozi wa bunge haswa kuhusu jinsi wanahabari wenye umri mdogo huvalia kwani mavazi yao huwa sio ya heshima,” akaelaza.

Bi Nyamai alitetea kauli yake akisema kuwa bunge kama asasi lina watu wenye heshima, wakiwemo wazazi. Lakini hakusema lolote kuhusu kanuni kuhusu mavazi na wajibu wa idara ya ulinzi bungeni katika kuhakikisha kuwa kila anayeingia humo amevalia nadhifu.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza la Vyombo vya Habari Nchini (MCK) David Omwoyo, ambaye alikuwepo katika mkutano, aliahidi kuwasilisha malalamishi ya wabunge kwa wamiliki wa vyombo vya habari.

Hata hivyo, Bw Omwoyo alielekeza kidole kwa wabunge akisema baadhi yao ni wamiliki wa vyombo vya habari na hukosa kuwalipa wanahabari, hali inayofanya baadhi yao kiuka maadili ya taaluma ya uanahabari.

“Baadhi yetu hapa ni wamiliki wa redio, televisheni na vyombo vingine vya habari. Wengine wenu mlikoma kuwalipa wanahabari baada ya kutamatika kwa uchaguzi mkuu.

Bila shaka hali hii ndio imechangia matatizo hayo ambayo mwaangazia hapa leo (Jumatano). Lakini kama MCK tufuatilia masuala hayo na wamiliki wa vyombo hivyo,” akaeleza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *