Hatimaye mradi wa wakuwapa wanafunzi wa shule za umma jimboni nairobi chakula unatarajiwa kuanza jumatatu ya tarehe 28 mwezi agosti mwaka huu 2023
Mradi huo ambo ni miongoni mwa ajenda kuu za gavana wa nairobi Johnson sakaja unatarajiwa kuwafaa zaidi ya wanafunzi laki 250 kutoka shule za msingi za umma zilizo jimboni nairobi.
“Huu mradi utasaidi sana kuimarisha viwango vya elimu nairobi” Gavana Sakaja alisema wakati wa uzinduzi wa jiko la kupikia chakula cha wanafunzi hao katika shule ya msingi ya Githurai.
Kwenye Mradi huo wa jina “DishCounty” serikali ya nairobi imetenga shilingi bilioni 1.7 ambapo shilingi milioni 500 zilitengea kujenga majiko ya kupikia chakula hicho cha wanafanzi huku nao mwanafunzi anatakiwa kutoa shilingi tano kugharamikia chakula cha mchana huku nayo serikali kuu na ile ya kaunti ya nairobi sawa na wahisani wakishirikiana ilikufanikisha.