Nambale: Odinga Ashtumiwa Kumpa Okwara Tiketi ya Moja Kwa Moja

Kindly read and share to support us reach our target audiences.
  • Wapiga kura wamekashfu vikali hatua ya Odinga kutowapa nafasi wachague wanayemuenzi
  • Baadhi yao wametishia sharti Bwana Geoffrey Mulanya awawakilishe katika bunge mwakani
  • Wengine wakiwa na mabango wanadai kufuza chama cha chungwa somo na badala yake kuchagua naibu raisi William Ruto

Shughuli za usafiri pamoja na usafiri zimetatizika mjini Nambale kwenye Barabara kuu ya Mumias Busia Baada ya baadhi ya wafuasi wa chama Cha ODM kuandamana kulalamikia hatua ya uongozi wa chama hicho kwa kutoa tiketi ya moja Kwa moja Kwa mmoja wa wawaniaji wa wagombezi wa ubunge

Wafuasi hao wa Wakili Geoffrey Mulanya wameandamana kutoka mjini Nambale hadi Mungatsi wakimkashifu kiongozi wa chama hicho Raila Odinga Kwa kumkabidhi Kevin Okwara tiketi hiyo hapo Jana katika ukumbi wa Bomas hapo Jana bila kushiriki mchujo.

Wafuasi hao wanadai kuwa Mulanya aliongoza Kwa umaarufu kwenye kura za maoni zilizoendeshwa na chama hicho,na kushangaa mbinu ambayo ODM ilitumia kumteua Okwara na kumkabidhi tiketi ya moja Kwa moja.

Baadae waandamanaji hao wamefululiza hadi katika afisi ya chama hicho hatua chache kutoka mjini humo na kuindoa maandishi ya chama hicho,huku wakitangaza kumuunga mkono Naibu wa Raisi William Ruto kuwa Raisi wa Agost,huku wakimtaka Mulanya kuwania kitu hicho Cha Ubunge Cha Nambale kama mgombea huru