Maafisa wa Polisi katika eneo Bunge la Navakholo Kaunti ya Kakamega wanamzuilia mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 31 ambaye anaishi na virusi vya UKIMWI, kwa tuhuma za kumbaka mwanawe wa miaka tisa na kisha kutupa mwili wake kwenye lango kuu la kuingia kwa boma la babake.
Babake mshukiwa, Henry Masinde, na mamake, Lidya Wawire, wanadai kuwa mshukiwa Martin Sifuna Wafula anadaiwa kumfukuza mkewe nyakati za usiku kwa madai kuwa alikuwa amemnyima haki yake ya ndoa kabla ya kumgeukia mwana wake wa miaka tisa, mwanafunzi wa darasa la pili, na kisha kumuua kinyama.
OCPD wa Navakholo, Richard Omanga, amehoji kuwa mshukiwa anaendelea kuzuiliwa akitarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.